Kabudi hawezi kutufundisha kuhusu siasa. Hana Achievement yoyote kwenye siasa afadhali hata Ntobi.
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Prof. Palamagamba Kabudi, amewataka viongozi na wanachama wa vyama vya siasa kuheshimiana katika kueleza tofauti zao za kisiasa, akisema matumizi ya lugha kama kumuita kiongozi mwenzake ambaye amechaguliwa “haramu” sio sahihi.
Prof. Kabudi amesema hayo leo Oktoba 7, 2026 katika Uzinduzi wa Uongozi Mpya na Nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika hoteli ya Hyatt-Regency jijini Dar es Salaam ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi
“Huwezi kumwita mwenzako kiongozi haramu, unaweza kusema hayupo hapo kihalali. Neno haramu katika Kiswahili lina maana ya ukakasi mkubwa sana,” amesema Prof. Kabudi.
Aidha, Prof. Kabudi amesisitiza umuhimu wa Baraza la Vyama vya Siasa kushirikisha wanawake na wadau wengine katika shughuli zake, akieleza kuwa heshima na ushirikiano ni sehemu muhimu ya kujenga mazingira mazuri ya kisiasa nchini.