Meli ya MV Liemba ni miongoni mwa meli kongwe zaidi za abiria duniani, ikiwa na historia ya zaidi ya karne moja katika Ziwa Tanganyika. Iliundwa nchini Ujerumani mwaka 1913 na awali iliitwa Graf von Götzen.
Wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia, meli hii ilitumiwa na Wajerumani kama chombo cha kijeshi katika Ziwa Tanganyika.
Mwaka 1916, ilizamishwa kwa makusudi na Wajerumani ili isiangukie mikononi mwa maadui wao. Baadaye iliopolewa, ikafanyiwa ukarabati na kurejea katika huduma mwaka 1927 kwa jina la MV Liemba.
Kwa miaka mingi, meli hii imekuwa kiungo muhimu cha usafiri wa abiria na mizigo kati ya bandari ya Kigoma, maeneo mbalimbali ya mwambao wa Ziwa Tanganyika na Mpulungu nchini Zambia. Imechangia kurahisisha biashara na usafiri kwa jamii zinazozunguka ziwa hilo.
Gustav Adolf Graf von Götzen alikuwa afisa wa kijeshi, mpelelezi na gavana wa Kijerumani aliyesimamia koloni la Afrika Mashariki ya Kijerumani, ambalo lilijumuisha sehemu kubwa ya Tanzania ya sasa.
Mwaka 1894 Aliongoza msafara wa Wajerumani uliovuka Rwanda, akiwa miongoni mwa Wazungu wa kwanza kurekodiwa safari ya kuvuka eneo hilo.
Hivyo Meli hii ilipoundwa nchini Ujerumani mwaka 1913, ikapewa jina Graf von Götzen kwa heshima yake.