VIONGOZI NA WANACHAMA 41 WA CHADEMA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KESI ZA UGAIDI
leo September 14, Mashauri saba dhidi ya viongozi na wanachama 40 wa chadema yametajwa huku shauri moja la Uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe Lissu likiendelea kwa hatua ya utetezi.
Mkoani Shinyanga, Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Shinyanga imeahirisha shauri namba 16506/2026, Jamhuri dhidi ya Jackson Rashid Mnyawami. (Ikumbukwe kuwa Jackson Mnyawami ni Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti )
Mashauri mengine dhidi ya wanachama yaliyoahirishwa mahakamani hapo ni pamoja na shauri namba 16503/2926 Jamhuri dhidi ya Jackson Venant Kabyeseleza, Shauri Na. 16505 Jamhuri dhidi ya Daniel Emanuel Athuman, Shauri Na. 16504/2026 Edwin Otieno Ongito na wenzake 8 na shauri namba 16506/2026 Jamhuri dhidi ya Godwine Laurent na wenzake 4.
Mashauri yote haya yameahirishwa hadi tarehe 25/09/2026 huku viongozi na wanachama 17 wakirejeshwa rumande kwa kuwa makosa ya Ugaidi wanayotuhumiwa nayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
Mkoani Mwanza, mashauri mawili yametajwa leo mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanaza, ambapo jumla ya wanachama 23 walipandishwa Mahakamani.
Shauri la kwanza ni Shauri namba 16375/2026 Jamhuri dhidi ya Deys E. Masalago na wenzake 09 na shauri la pili ni Shauri namba 16379/2026 Jamhuri dhidi ya Fantson Wilson Nyamwanga na wenzake 12.
Mashauri yote mawili yameahirishwa hadi tarehe 28/09/2026 yatakapo tajwa tena huku watuhumiwa wote wakirejeshwa gerezani kwa kuwa makosa ya ugaidi hayana dhamana kisheria.
Nawashukuru mawakili waliofika mahakamani kwa upande wa utetezi, Wakili Erick Mutta, Wakili Fellan Kweka, Wakili Sijaona Revocatus na wakili Gibson Ishengoma.
Mkoani shinyanga pia wakili Aloyce Kajitamus nakushukuru kwa kusimama upande wa utetezi.
Viongozi na wanachama waliopandishwa kizimbani leo jumla yao ni 41, ambao ni mwenyekiti Taifa Mhe Lissu (Uhaini) Shinyanga -17 (Ugaidi) na Mwanza (23) Ugaidi.
Taarifa na mwendelezo wa shauri dhidi ya Mhe Lissu utawaajia baadaye, kwa sasa shauri linaendelea Mahakama kuu, Masijala ndogo ya Dar Es Salaam.