Mtu mmoja, anayedaiwa kuwa raia wa kigeni, amefariki dunia na watu wawili kujeruhiwa baada ya Toyota Alphard, lenye namba T 837 EMS, kugongana uso kwa uso na basi la ZUGSPITZE Express, lenye namba T 636 AQN, eneo la King’ori, Arumeru mkoani Arusha.
Mashuhuda wamesema ajali hiyo imetokea leo, Agosti 8, 2026, majira ya asubuhi, huku mmoja wa abiria, Recho Ali, akidai dereva wa basi hilo hakuwa mzoefu na alikuwa akifundishwa kuendesha kabla ya ajali kutokea.
"Dereva huyu hakuwa mzoefu kulikuw ana mwenzake ambaye alikuwa anamfundisha kuingiza Gia na Kutoa akipatia anamwambia hapo sawa, sasa Kulikuwa na Abiria amekaa pembeni akamwambia kwanini usiendeshe wewe kama huyu hajui vizuri, akagoma kujibu akanyanyuka akaanza kudai Nauli, tukaambizana tukikutana na askari tumweleza, ghafla nikasikia Mlio, kumbe tumepata ajali" - Anasema Recho Ali abiria aliyekuwa akisafiri kuelekea mkoani Kilimanjaro.
Basi hilo lililokuwa likielekea Tanga limeteketea kwa moto, huku Toyota Alphard likiwa linaelekea Arusha mjini.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limethibitisha kifo cha mtu mmoja katika ajali hiyo.