Makamu wa Rais Ndejembi kwa Waziri Mkuu Mwigulu kuhusu mifumo kutokusomana: 'Bado tupo nyuma'
“Maelekezo ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo amekuwa akiyatoa mara kwa mara ya kutaka mifumo isomane, bado tupo nyuma Msheshimiwa Waziri Mkuu. Huku kuna ‘YES’ mfumo mzuri kabisa, huku kuna ‘Kazi Portal’ kama sikosei Mheshimiwa Sangu, nayo ‘Kazi Portal’ kijana huyuhuyu anayejisajili ‘YES’ anatakiwa na yeye tena huyu huyu aingie ‘Kazi Poratal’ lakini huyu huyu kijana aliyehitimu wakati anatafuta ajira ya kuingia katika Utumishi wa Umma tunamwambia pia aingie ajisajili ‘Ajira Portal’. Serikali moja, mifumo mitatu ambayo tunamtaka huyu kijana atumie kifurushi chake," amesema Ndejembi.