True story!.
Siku moja nikiwa form two mkoani morogoro.
Mzee wangu alinishonea suruali ya shule safi Tu ambayo ilikuwa ni (MAMA NCHANULIE).
Kwa akili za utoto na ujana,nikaichukua na kwenda kuitengeneza kuwa modo.
Asubuhi niliamka na kwenda shule lakini Baba hakuniona,Niliporudi tulikutana mlangoni ndipo akaanza kuongea.
He said"YANI SURUALI NIMEKUCHONEA JANA LEO UMEENDA KUIFANYA UNAVYOTAKA".
Nikajichanganya kumjibu kuwa ndio,inanifanya nakuwa smart.
He said"Nenda kavue halafu uniletee",bila kumpinga mzee wangu nikafanya hivyo.
Lakini nilishangaa kumuona mzee wangu akiichana na kusema sasa "Unaweza kwenda kushona unayotaka".
Nililia sana by that time sikuwa na chochote na ukizingatia ni mwanafunzi.
Kesho yake nilishindwa kwenda shule baada ya Mzee wangu kunichania suruali.
Hali iliyonifanya kuchukua makundi ya watu watano,siku hiyo kwenda kuchunga walau nipate hata 20k kwaajili ya kushona suruali mpya.
Muda ulipofika nilifungulia mbuzi na ng'ombe na kuingia zangu porini.
Nikiwa porini wingu kubwa lilitanda Angani kuonesha mvua kubwa inakuja kwa muda huo.
Kutokana na ile hali nikajiandaa walau kusogea upya karibu na kijiji jiran.
Lakini Ghafla matone ya mvua yalishuka na kuninyeshea kwa muda ule.
Mvua ilidumu kwa zaidi ya saa moja na nusu.
Baada ya hapo nikasogea karibu na makorongo ya maji walau kupata maji ya kukata kiu.
Niliangalia huku na huku nilikosa hali iliyonifanya,kuvua shati langu na kuliweka juu ya yale maji ambayo ng'ombe walikuwa wanakunywa.
NB:Hatuwezi kumheshimu mtu, ambae haoni thamani yetu licha ya magumu tuliyopitia,nidhamu ndio imetupa kibali cha kuendelea kuwa bora.