UTANGULIZI KUHUSU KESI YA MHE. LISSU.
Leo siku ya Jumatatu, February 16, 2025 Tuko Mahakama Kuu tena, Wanapaita Muembeni, Dar es salaam Tanzania.
Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa Tundu Lissu.
Leo tunatarajia kumsikiliza Shahidi wa 7 (PW7) kati ya mashahidi 30 wa Jamhuri ambao wamekwisha kutoa ushahidi mbele ya Mahakama hii.
Hadi leo tumeshuhudia vielelezo vinne vya upande wa Utetezi vikipokelewa na Mahakama lakini upande wa Washitaki yaani Jamhuri hawajasilisha kielelezo chochote ambacho kimepokelewa.
Ikumbukwe huko nyuma walijaribu kuwasilisha vielelezo ambavyo ni pamoja na ile video iliyokataliwa na Mahakama ambayo Mh. Tundu Lissu alikuwa anazungumza maneno aliyoshtakiwa katika kesi hii pia ilikataliwa ripoti ya mtaalamu aliyefanya uchunguzi video hiyo.
Hali ya Mahakama ni nzuri na muda wowote Mh. Tundu Lissu ataingia Mahakamani. Waandishi wa Habari wako rada na Camera zao. Umakini wao huwa ni mkubwa sana wakati Mh. Lissu anaingia Mahakamani na kutoka.
Nafikiri wanauza sana picha na video za vionjo vya Mh. Tundu Lissu hasa akiwa anaingia Mahakamani hapo kizimbani.
Kuna muda asipoongea huwa wanamchokoza wao wenyewe ilimradi aseme neno lolote. Bahati nzuri kila neno la Mh. Tundu Lissu huwa lina maana sana na lazima liende Mjini😂
Nawaona walivyojazana kizimban, wako makini sana ni muda ambao kila aliyeshika camera huwa hapepesi hata macho.
Mawakili wa Serikali leo wamewahi saa tatu na dakika 5 walikuwepo tayari Mahakamani. Walivyowahi unaweza kudhani kuna jambo la maana wamejiandaa nalo lakini mashahidi wao wakianza kutoa ushahidi ndio lazima uchoke.
Hapa katika Chumba cha Mahakama wako wafuatiliaji wa kesi wanakaa eneo la juu. Hawa wao ni watu wenye vibe sana. Wanapaita Gaza kule walipokaa.
Kama mnamkumbuka yule Mtumishi wa Mungu aliyesema ana Ujumbe kutoka kwa Mungu kuwa Mh. Tundu Lissu aachiwe haraka na Majaji walijue hilo. Sasa na yeye ndio alikuwa amekaa huko juu na alikuwa anayazungumza hayo akitokea huko Gaza ndani ya Ukumbi huu Na. 01 hapa Mahakamani.
Muda wowote kesi itaanza.