Ukiniuliza mimi, nitakwambia game ya chadema vs wanaharakati iko so tricky and kind’f complicated.
Kuna mmoja hapo anakuwa driven na hisia kuliko uhalisia wa siasa.
Chadema ni chama cha siasa, lengo lake kuu ni kushika dola, agenda yake kuu ni kupinga,kukosoa na kushauri serikali (chama tawala)
Kwenye hizo agenda kuu sasa ndo kuna tricky hapo, chadema inampasa kujiuza kwa wapiga kura kwa kuwaambia kuwa sisi hatuko hivo kama wao watawala na tukishika dola hatutayafanya haya na yale wanayofanya hawa watawala!!
Hatutaua, kwaio inabidi wasiue hata sasa.
Hatutaiba, inabidi wasiibe hata sasa.
Hatutafurahia tukiona binadamu amekufa au ameuliwa hata akiwa ni adui!! Na inabidi waanze kuonyesha hayo sasa.
Adui akifa au akifiwa tutaenda kuzika na tutaenda kuhani msibani!!
Yote haya ni ili chadema asionekane yeye naye ni roho mbaya tu kama alioko kwenye kiti!!
Kwahiyo chadema unakuta ana jukumu la kumpenda hadi adui ili kuonyesha watu kuwa sisi hatuko hivyo.
Otherwise mpiga kura ataona aaah mtawala wa sasa ni mkatili, lakini mbona hata huyu chadema nayeye anaonekana ni mkatili kabla hata hajashika dola!!🤔 Huyu akishika dola si ndio atakuwa katili zaidi ya wa sasa!!
Finally mtu anaamua bora shetani wa zamani niliemzoea kuliko shetani mpya!!
But kwa wanaharakati sasa ni tofauti…. hisia zinawapush wawe na mentality ya ngadu kwa ngadu,
🦷 kwa 🦷, mwaga bapa namwaga kichanganyio!!
Anayekuua na kukuteka na kukutesa, siku nayeye akifa angusha party kihomeboy shangilia!!
Its very complicated hii game!!
Ndo yale yale nasemaga, kama unamkosoa kiongozi wa chadema kwenye comment then akakublock means huyo siku akiwa tu DC ukakosoa anakutia ndichi masaa 72!!
Ni lazima anayempinga mtawala asiwe na characters za mtawala!!
Sijui kama niko sahihi au nimeamka na wenge!!