VIDEO:
Wananchi mkoani Iringa wametakiwa kuepuka kujichukulia sheria mkononi wanapokumbana na migogoro ya mahusiano, huku wakihimizwa kuripoti vitendo vya jinai polisi badala ya kuvificha kwa sababu ya huruma.
Wito huo umetolewa Oktoba 12, 2026, na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Iringa, ASP Elizabeth Swai, wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni ya Ongea na Kamanda uliofanyika Kata ya Kitwiru, Manispaa ya Iringa.
Swai amesema wananchi wanapaswa kutoa taarifa mapema kuhusu matukio ya jinai yanayotokea katika mahusiano ili yaweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria, badala ya kutumia nguvu au kuchukua hatua nje ya utaratibu wa kisheria.
Akifafanua majukumu ya Dawati la Jinsia na Watoto, amesema dawati hilo si chombo cha kusuluhisha migogoro ya kimahusiano, bali ni sehemu yenye usiri ndani ya Jeshi la Polisi inayopokea na kushughulikia masuala ya jinai yanayohusiana na mahusiano kwa mujibu wa sheria.