Akili ni mali.
Tanzania ina vipaji na ari ya kuchangia katika kuunda mustakabali wa kidijitali wa Afrika, na si kuwa mtumiaji tu wa teknolojia.
Kaimu Balozi Andy Lentz alitoa hotuba leo katika tamasha la tano la Data Tamasha linalofanyika kila baada ya miaka miwili, lililoandaliwa na Tanzania Data Lab (dLab).
Tamasha hilo linaangazia jinsi data, akili bandia (AI), na teknolojia ya kidijitali zinavyoweza kupanua fursa za kiuchumi na kuchangia mustakabali wa kidijitali wa Tanzania.
dLab ina uhusiano wa muda mrefu na Marekani, na kwa pamoja, kwa kutumia teknolojia bora zaidi ya Marekani, tunaweza kujenga mfumo wa ubunifu uliounganishwa kimataifa ambao ni salama kwa watumiaji.