Mtu anieleweshe nchi ndogo kama Zanzibar inakuwaje na Wizara 20 jaman !!
Imagine mawaziri 20, Manaibu mawaziri 20, Makatibu Wakuu 20, manaibu Katibu Wakuu 20.... wanapewa magari mazito, ofisi, posho na marupurupu.
Kwa uchumi gani Zanzibar hadi wafanye hivyo?
Mawaziri wanne kutoka ACT-Wazalendo wameteuliwa katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar, baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, kufanya mabadiliko ya Baraza hilo lenye wizara 20.
Mawaziri hao ni Nassor Ahmed Mazrui anayekuwa Waziri wa Afya, Omar Said Shaaban anayekuwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Nasra Nassor anayekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale na Dkt. Mohamed Ali Suleiman anayekuwa Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu.
Uteuzi huo umefanyika baada ya maridhiano na makubaliano kati ya CCM na ACT-Wazalendo yaliyowezesha pia kuteuliwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman, pamoja na wawakilishi wawili wa viti maalumu, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Akizungumza Ikulu Zanzibar leo Oktoba 3, 2026, Dk Mwinyi amesema mabadiliko hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika utendaji wa Serikali, huku akisisitiza kuwa kukamilika kwa uundaji wa SUK kutaiwezesha Serikali kuelekeza nguvu katika amani, umoja na maendeleo ya wananchi.
Katika mabadiliko hayo, Dk Saada Salum Mkuya ameteuliwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Masoud Ali Mohamed ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu, huku Mudrik Ramadhan Soraga akiteuliwa kuwa Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi. Aidha, Shaaban Ali Othman ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu na Ali Suleiman Mrembo kuwa Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.
Rais Mwinyi pia ametangaza mabadiliko kwa baadhi ya manaibu mawaziri, huku sekta ya Mipango ikihamishwa kutoka Wizara ya Fedha kwenda Ofisi ya Rais na sekta ya Kazi ikiunganishwa na kuunda Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.
Dk Mwinyi amesema Kamati ya Pamoja ya Mazungumzo imeundwa kwa ajili ya kujadili na kutatua changamoto au vikwazo vinavyoweza kujitokeza katika utekelezaji wa mfumo wa SUK, akieleza kuwa matarajio makuu ya Serikali hiyo ni kudumisha amani na umoja na kuelekeza nguvu katika maendeleo badala ya marumbano ya kisiasa.