Mudathir na Mabula wote wanatembea zaidi. Kama unatawala mechi ni wazuri, watakusaidia kushambulia zaidi. Ila kama timu yako ni underdog ambao wanashambuliwa zaidi au unataka kutumia DM moja pekee bado Himid atacheza tu.
Taifa Stars sio Simba, Yanga au Azam. Taifa Stars ni underdog kwenye mechi nyingi.
Mechi dhidi ya Guinea Bissau, Gamondi aliingia kwa lengo la kushambulia zaidi ndio maana akaweka DM mmoja, Himid na tukashambulia vizuri, tatizo likawa kushindwa kutumia nafasi.
Mechi ya Madagascar akaamua kutafuta mzani wa kushambulia na kujilinda akaanza na DM wawili, Himid na Mabula. Kwa sababu Himid analinda zaidi, Mabula anakuwa na nafasi ya kwenda mbele.
Kwenye AFCON 2025, ilibidi Gamondi atumie viungo watano kwa sababu hatukuwa na DM mwenye uwezo wa kutupa defensive cover kihivyo. Nova na Mabula wote ni passers zaidi sio watu wa kupoka mipira au kunusa hatari.
Sawa lakin Muda sasa yupo fit, sidhani kama Himid atakupa uhakika katika mechi kuliko Muda, Jana kuna mda ilibidi Mabula arudi chini Mao asogee Juu, ambapo uwezekano wa muda kutimiza majukumu hayo ni makubwa kuliko Himid.