Tanzania's third largest opposition party according to GoT and its allies Ngogwe and ubwabwanomics 🍚
Hilda Newton
4
12
67
1,926
#TANZANIA: MAMBO YA KISIASA, TUMALIZE KISIASA, TUNATAKA UKWELI NA UWAJIBIKAJI, HUWEZI KUUWA WOTE - MWABUKUSI Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi leo Oktoba 07, 2026 akizungumza kayika baraza la vyama vya siasa lililofanyika jijini Dar Es salaam ametoa mapendekezo ya kuanzishwa kwa kamati maalum chini ya sheria ya vyama vya siasa itakayoshughulikia makosa na migogoro inayotokana na masuala ya kisiasa. Mwabukusi amesema masuala ya kisiasa yana mazingira na lugha yake, hivyo yanapaswa kushughulikiwa kwa kuzingatia muktadha huo kabla ya kupelekwa katika mifumo mingine. Aidha, Mwabukusi amesisitiza umuhimu wa vyama vya siasa kuvumiliana licha ya tofauti zao, akieleza kuwa siasa zinahitaji nafasi kwa watu wenye mitazamo tofauti kuishi, kujadiliana na kutafuta suluhu kwa njia ya mazungumzo. Zaidi: youtu.be/drd9y5KrsCs
4
19
77
3,229
MAHAKAMA KUU KUTOA UAMUZI KESHO KESI YA MAOMBI YA SAID ISSA MOHAMED DHIDI YA CHADEMA. Kesho tarehe 8 Oktoba 2026 Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam itatoa Uamuzi juu ya Maombi ya Zuio katika Maombi Madogo Namba 14864 ya 2026 baina ya Said Issa Mohamed & Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Registered Trustees of Chama cha Demokrasia na Maendeleo & Secretary General of Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mnamo saa 8 na Nusu Mchana. Wanachama na viongozi mnaombwa kufika kwa wingi kusikiliza uamuzi huo. Haya ni maombi mengine ambapo waombaji wanaomba Mahakama kuu kufungia Chama kwa Mara nyingine tena.
2
23
71
1,427
Jm retweeted
Sarafina baada ya kutoka Gerezani na wenzake baada ya MATESO makali alijuliza maswali mawili. 1. Walitukamata na kututesa tuwe kama wao? 2. Walitukamata na kututesa ilituwaogope? Baada ya hapo miezi 18 MANDELA akaachiwa huru na UKOMBOZI ukapatikana. Vijana hawakunyamaza kabisa, licha ya mateso yote waliyopitishwa na MAKABURU. MAKABURU WETU LEO NI WAKOLONI WEUSI. Wanatuteka na kututesa kila siku bado mapambano yanaendelea. Tunaamini ushindi upo karibu UNAKUJA. TUTAKUWEPO🫵🏾😎
3
37
240
5,629
Leo viongozi na wanachama 17 wakiongozwa na Katibu wa Kanda ya Serengeti Jackson Rashid Mnyawami wamepandishwa kizimbani, Mahakama ya Hakimu mkazi wa Mkoa wa Shinyanga dhidi ya mashitaka ya Ugaidi yanayowakabili. Mashauri ya leo ni pamoja na Economic case namba 16506/2026 inayomkabili Jackson Rashid Mnyawami, Mashauri mengine ni Economic Case No. 16503/2026, inayomkabili Jackson Venant Kabyeseleza, Economic Case No. 16504/2026 Inayomkabili Edwin Otieno Ongito na wenzake 8, Economic Case No. 16505/2026, inayomkabili Daniel Emanuel Athuman , Economic case namba 16506/2026 inayomkabili Laurent na wenzake 4.
34
114
2,628
Jm retweeted
Asante sana Tarime .. Nyie ni watu wema sana . Ninawapenda sana . Katiba mpya ni sasa Free Tundu Lissu.
6
135
723
13,824
PUBLIC STATEMENT @IPUparliament
6
65
170
5,587
"Wewe bwana Afande" wamenuna walivyosikia hizo hesabu 😂😂
10
29
178
12,152
Mratibu wa Chaso Mkoa wa Mwanza Tumsaidie wapendwa ili aweze kumaliza elimu yake ya chuo kwani ametengwa na familia yake kwa sababu ya kuwa mwanachadema na kusimamia upande wa haki
12
83
216
4,652
Tishio hili dhidi ya mwenyekiti wa Bavicha taifa kamanda @AdvMahinyila tumelipokea kwa uzito mkubwa. Hatupuuzi hata kidogo, lakini msijaribu kufanya huu upumbavu.
11
97
383
7,866
kwa vijana wote wenye akili na karama zinazowawezesha kufanya vitu vingine lakini wakaamua kuingia kwenye siasa, hususan za upinzani, asanteni sana. nyinyi ndo tumaini la taifa hili, na tunashukuru kwa kujitoa kwenu:
9
118
557
5,982
National security inageuka kuwa regime security pale ambapo taasisi zilizoundwa kulinda taifa zinaanza kutafsiri usalama wa walioko madarakani kuwa sawa na usalama wa taifa. Tofauti hiyo inaweza kuonekana kwa vipimo hivi: 1. Ukosoaji unapogeuzwa kuwa tishio la kiusalama. Mwananchi anayemkosoa Rais, Serikali au chama tawala anaanza kutazamwa si kama mkosoaji wa kisiasa bali kama mtu anayehatarisha taifa. 2. Upinzani unapogeuzwa kuwa adui wa dola. Kushindana na chama tawala, kutaka kukiondoa kupitia uchaguzi au kudai mabadiliko ya Serikali kunaanza kutafsiriwa kama kuhatarisha nchi. 3. Vyombo vya usalama vinapoanza kulinda political survival ya watawala. Badala ya kuuliza “Tanzania iko salama?” mfumo unaanza kuuliza “Serikali hii itaendelea kuwa madarakani?” 4. Sheria za usalama zinapotumika kusimamia migogoro ya kawaida ya kisiasa. Masuala yanayopaswa kujibiwa kwa hoja, uchaguzi, Mahakama au siasa yanaanza kushughulikiwa kama masuala ya usalama wa taifa. 5. Maslahi ya chama yanapochanganywa na maslahi ya taifa. Hapo kumpinga chama tawala kunaanza kuonekana sawa na kuipinga nchi. 6. Kulinda kiongozi kunapokuwa muhimu kuliko kulinda taasisi. Rais au Serikali inaanza kulindwa dhidi ya accountability badala ya Urais na Serikali kulindwa kwa kuhakikisha zinafanya kazi ndani ya Katiba. 7. Taifa linapoanza kuogopa mabadiliko halali ya madaraka. Uchaguzi unaanza kutazamwa kama salama ikiwa chama tawala kinashinda, lakini uwezekano wa kushindwa kwake unaonekana kama instability au security threat. Kipimo rahisi kabisa ni hiki: National security hulinda mfumo ambao unaweza kubadilisha watawala. Regime security hulinda watawala dhidi ya mfumo unaoweza kuwabadilisha. Kwa hiyo national security yenye afya inaweza kuilinda Serikali dhidi ya mapinduzi, ugaidi au uvamizi—lakini wakati huohuo ilinde haki ya wananchi kuiondoa Serikali hiyo kwa kura. Siku vyombo vinapoanza kuona kupoteza madaraka kwa watawala kama kupoteza usalama wa taifa, hapo mstari umevukwa: national security imeanza kuwa regime security.
4
47
147
3,606
Jm retweeted
Hii ni TARIME wananchi wanataka KATIBA MPYA na LISSU aachiwe. Hii nyomi inawaumiza sana WAKOLONI WEUSI. Chama kinaendelea kupendwa kila kona ya NCHI. Repost 200
3
100
479
5,989
Jm retweeted
Mvua imenyesha sana watu wamesimama mwanzo mwisho kumsikiliza MAKAMU HECHE. Haya ni zaidi ya mapenzi, Asanteni watu wa TARIME.❤️🫶 Repost 200
John Heche
6
183
1,037
11,539
Jm retweeted
Tarime asante sana, Pamoja na kunyeshewa sana mmesimama imara kwaajili ya ukombozi wa Nchi yetu. Tunataka katiba mpya. Tunamtaka Mwenyekiti wetu aachiwe haraka.
19
194
728
22,892
Asanteni sana Tarime ✌️
8
91
529
24,903
#TANZANIA: TUNATAKA LISSU AACHIWE, NI MTU MWEMA, MTU MWENYE AKILI KWAO NI TISHIO - HECHE Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche leo Oktoba 06, 2026 alipokuwa akiwahotubia wananchi wa Tarime Mjini amesema Tundu Lissu ni mtu mwema wanatakiwa kumuachia huru, "mtu mwenye akili kama Lissu ni tishio kwa watawala, tunataka mwenyekiti wetu aachiwe na tunataka katiba mpya" Zaidi: youtu.be/h1AuzaXHqSM
1
33
80
2,883
Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti Bara Mhe @HecheJohn Tarime akiingia Uwanja wa Shamba la Bibi
10
113
545
51,283
#TANZANIA: NILIITWA POLISI LEO, SISI HATUPO KUTOA KAULI ZA KUIFURAHISHA CCM WALA KUIFURAHISHA SERIKALI - MAHINYILA Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa (BAVICHA), Wakili Deogratias Mahinyila leo Oktoba 06, 2026 amesema ni kweli aliitwa na Jeshi la Polisi Tarime na kusema kuwa wao hawapo kuifurahisha CCM wala serikali. Aidha, Mahinyila amesema kauli walizozitoa za viongozi wa CCM hazijawahi kuchukuliwa hatua yoyote ile na jeshi la Polisi akitolea mfano wa Mwenyekiti wa UWT kuwa aliwahi kusema kama Rais Samia angempa nafasi hata dakika moja angehakikisha anawamaliza upinzani wote lakini hajawahi kuchukuliwa hatua yoyote. Zaidi: youtu.be/m38nP2oXLtA
3
56
191
5,340
Katika mfumo wa haki jinai unaofuata misingi ya utawala wa sheria, jukumu la msingi la upande wa mashtaka ni kuthibitisha tuhuma dhidi ya mshtakiwa bila kuacha shaka (beyond reasonable doubt) Katika kuthibitisha prima facie evidence upande wa mashtaka, tulitarajia kushuhudia ushahidi wa kina (substance) unaothibitisha vipengele vya kosa la uhaini kabla ya mshtakiwa kuamriwa kujitetea Kuamua ikiwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu, Mahakama inapima iwapo Jamhuri imewasilisha ushahidi wa kina (substance of evidence) kuthibitisha kosa (ingredients of the offence) Jopo la majaji watatu walisema wao hawakujikita katika uzito wa ushahidi (substance of evidence), bali walizingatia tu kama Jamhuri imeeleza mashtaka yake kwa uwazi (clearly stated charges) Wafuatiliaji wa kesi na wadau wa sheria waliona ni kama mbinu ya kukwepa uwajibikaji wa kiufundi (escapism). Ruling on No Case to Answer haikuwa na uzito unaostahili to put the accused on defense Hii inaondoa maana halisi ya kiwango cha uamuzi wa prima facie evidence na inaleta mashaka iwapo uamuzi ulilenga kumpa mshtakiwa haki au ulilenga kumlazimisha kujitetea bila msingi wa kisheria Kosa la Uhaini ni miongoni mwa makosa mazito zaidi katika sheria zetu za jinai, ambalo linabeba adhabu ya kifo (kunyongwa hadi kufa) endapo mshtakiwa atapatikana na hatia mbele ya Mahakama Katika majumuisho ya mwisho (final submission), Jamhuri walisema kuwa matumizi ya neno “liable” katika kifungu cha sheria yanaipa Mahakama utashi (discretion) wa kutoa adhabu mbadala Wakaeleza kwamba Mahakama inaweza kutoa adhabu kuanzia kifungo cha miaka sifuri hadi adhabu ya kifo. Wakafafanua kwa kueleza tofauti ya “shall be sentenced to death” na “liable to suffer death” Mantiki inayojitokeza hapa ni kwamba Jamhuri inamshtaki Tundu Lissu kwa kosa la Uhaini, adhabu ni kifo au kuachiwa huru, lakini wakati huo haitaki adhabu ya kifo itolewe kwa mtuhumiwa Kuna kila sababu ya kuchanganua ni kwanini Mawakili wa Serikali ambao wanawakilisha Jamhuri waonyeshe uelekeo wa kuomba adhabu mbadala au nafuu badala ya adhabu hiyo ya kisheria Ombi hili la adhabu nafuu halisukumwi na huruma ya Mawakili wa Serikali. Hawana huruma. Bali, ni ishara ya wazi kuwa Jamhuri inatambua udhaifu mkubwa wa ushahidi wake uliowasilishwa mahakamani Hii inatueleza kiwango cha ushahidi wa Jamhuri kilichowasilishwa hakikutimiza kizingiti cha zaidi ya shaka inayostahili (beyond reasonable doubt) kinacholindwa na Ibara ya 13(6)(b) ya Katiba Hata wao wanaelewa, hakuna ushahidi wa kosa la uhaini waliowasilisha. Hivyo upande wa Jamhuri unajaribu kujenga mazingira ya kupunguza athari za kisheria endapo hukumu ya hatia itatolewa Ombi la adhabu nafuu kwenye kosa linalobeba adhabu ya kifo ni mkakati wa kuhakikisha mahakama inapata mianya ya kutoa hukumu ya hatia bila kuibua mtafaruku wa kisiasa ndani na kimataifa Mwenendo unazua hofu kuwa Mahakama inaweza kuendelea kufuata mwelekeo na matakwa ya upande wa mashtaka badala ya kusimama kama mhimili huru unaopima haki kwa uwazi na usawa Endapo mtiririko huu wa kupindisha kanuni za kisheria ili kubeba matakwa ya kisiasa utaendelea hivi, tutaendelea kushuhudia kushuka kwa viwango vya kitaalamu vya mhimili wa mahakama Kuporomoka kwa imani ya wananchi katika mifumo ya utoaji haki si jambo linalotokea bahati mbaya; ni matokeo ya haki kupindishwa mara kwa mara katika mamlaka zenye dhamana ya kutoa haki Mahakama inapochukuliwa kama chombo cha kuratibu matakwa ya kisiasa badala ya kuwa ngome ya haki na ukweli, msingi wa amani, utawala wa sheria unakuwa hatarini. Huu ni ukweli dhahiri Justice must not only be done, but must also be seen to be done – Haki haipaswi tu kutendeka, bali lazima ionekane wazi ikitendeka. Maneno ya Jaji Lord Hewart katika kesi ya Rex v. Sussex Justices (1924) Hii ni kanuni muhimu ya utawala wa sheria: haki haitoshi kutendeka; mchakato na mazingira ya uamuzi lazima pia yaonyeshe kwa uwazi kwamba haki imetendeka. Ndiyo msingi wa hoja yangu “You will never find justice in a world where criminals make the rules/law” MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
6
111
451
18,110